Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MWINYI : TUTAPANDISHA MISHAHARA KWA WATUMISHI KADRI UCHUMI UTAKAVYOIMARIKA



Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema Serikali itapandisha mishahara kwa watumishi wa kada ya kati kadri uchumi utakapozidi kuimarika.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Meimosi, 2021 katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-Wakil Kikwajuni, Zanzibar.

Amebainisha kuwa wafanyakazi hao ni muhimu katika maendeleo na ndio kada yenye wataalamu wakiwemo walimu na watumishi wa sekta ya afya.

Amesema Serikali ilikuwa na nia njema ya kuimarisha mishahara kwa wafanyakazi wa ngazi zote kwa awamu tatu, hata hivyo hatua hiyo ilishindwa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Amesema ugonjwa huo uliathiri ukusanyaji wa mapato hivyo utaratibu huo kuishia katika kuimarisha viwango vya mishahara ya kima cha chini hadi kufikia Sh300,000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com