Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC) Issaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za NIC leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Bima Marathon Bw.Baraka Mtavangu akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za NIC leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZTE NA EMMANUEL MBATILO
****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa mara nyingine amekuwa mdhamini mkuu wa Bima marathon zitakazofanyika Mei 29 mwaka huu katika Kiwanja cha Mlimani City Jijini Dar es Salaam ambapo kauli mbiu ikiwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Serikali kuondoa vifo vya watoto njiti na kuimarisha afya zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC) Issaya Mwakifulefule amesema kuwa NIC wamekuwa mstari wa mbele kusapoti mambo mbalimbali yenye lengo la kukuza ajira kwa vijana nchini na kulinda afya zao pamoja na kutengeneza mawasiliano hivyo Bima Marathon wana lengo hilo.
“Kuna makusanyo yanayopatikana kwenye kujiandikisha kwenye hizi mbio, sehemu yake inakwenda kupelekwa kwaajili ya kufariji watoto wetu waliozaliwa njiti katika hodi yao maalumu.NIC tuliona kupitia mbio hizi tushiriki kuweza kusaidia watoto hawa”. Amesema Bw.Mwakifulefule.
Aidha Bw.Mwakifulefule ametoa wito kwa watanzania kuendelea kujiandikisha kwa kujitokeza kwa wingi waje kushiriki mbio hizo kwani kushiriki kwao si tu watakimbia na kulinda afya zao lakini pia watasaidia watoto njiti waweze kufanikisha ndoto zao
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Bima Marathon Bw.Baraka Mtavangu amewashukuru NIC kwa kuweza kuwa wadhamini wao katika mbio hizo hivyo wamekuwa na mchango mkubwa hasa katika kuleta tabasamu kwa watoto njiti.
Hata hivyo amesema washiriki wote watakaoshiri watepewa tshirt na medali pamoja na mshindi wa kwanza atapewa milioni moja, mshindi wa pili atapewa laki saba na mshindi wa tatu atapewa laki tano hii ikimaanisha kwamba washindi wa kiume na washindi wa kike tuti ya kilometa 10 na kilometa 21.
“Katika kilometa 5 zawadi zote ambazo tumeziweka kwa mshindi wa kwanza atapewa laki mbili, mshindi wa pili laki moja na mshindi wa tatu elfu hamsini hii ni kwa watoto ambao watakuwa wamekuja kukimbia ama kutembea kwenye kilometa tano”. Amesema Bw.Mtavangu.