Msanii Ommy Dimpoz
Msanii Ommy Dimpoz yupo mjini Makka nchini Saudia Arabia, ameungana na waumini mbalimbali wakiislamu duniani kufanya ibada ya Umrah baada ya mwaka 2019 kushindikana kutokana na kuumwa.
Dimpoz amekuwa ni mtu wa ibada siku zote na kupitia ukurasa wake wa Instagram, ame-post picha kadhaa akiwa ndani ya msikiti jirani “Al-Ka'abah” ambao ni nyumba maalum ya Mwenyezi Mungu na kawaida wahudhuriaji huzunguka mara 7.
Makka ni mji mtakatifu wa Uislamu na kila mwaka mamilioni wa Waislamu wanahiji kwenda Makka.
Social Plugin