Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelekezo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kiwanda cha Kamel Steel Industry kinachozalisha nondo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua baadhi ya nyaya zilizotengenezwa na madini ya kopa kwenye kiwanda cha OK Plast Limited katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kiwanda cha OK Plast limited kinachotengeneza nyaya za umeme kwa kutumia madini ya kopa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na uongozi wa kiwanda cha OK Plast limited kinachotengeneza nyaya za umeme kwa kutumia madini ya kopa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo amekiagiza kiwanda cha Quaim Steel Mills limited kuhakikisha kufikia miezi miwili kiwe kimejitengenezea mkakati wa kuhakikisha moshi wa kiwanda hicho hautoki na kusambaa kusababisha uchafuzi wa mazingira.
Ameyasema hayo leo Mhe.Jafo mara baada ya kutembelea kiwanda hicho katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Jafo amewaagiza wenye kiwanda hicho kuhakikisha wanakifanyia marekebisho kiwanda hicho kwaajili ya kulinda afya za wananchi hususani ajenda ya utiririshaji wa moshi hivyo amewataka NEMC baada ya miezi miwili kufika katika kiwanda hicho na kukagua kama kimeshafanyiwa marekebisho.
"Kiwanda cha Quaim Steel Mills limited nimewapa miezi miwili waweze kufanya marekebisho makubwa katika kiwanda chao kwa lengo la kukidhi sheria ya mazingira no.20ya mwaka 2004". Amesema Waziri Jafo.
Aidha Waziri Jafo mewataka wenye viwanda nchini kuhakikisha wanazingatia afya za wananchi kwa kuhakikisha viwanda hivyo havitirirshi moshi ama maji taka ambayo yataenda kuathiri watanzania.
Hata hivyo Waziri Jafo amesema atakaa na kuzungumza na Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha wanavisaidia viwanda vya ndani viweze kufanya kazi vizuri na kuhakikisha mazingira yanatunzwa na vijana wa kiktanzania kupata ajira kupitia viwanda hivyo.