Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021katika Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa pamoja na Makamu wa Rais Dkt.
Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara, Philip Mangula, pamoja na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa
Mkutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumza na Wazee
wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021.
Viongozi wa Kidini,
Viongozi Wakuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wazee wa Mkoa wa Dar es
Salaam wakiwa wamesimama wakati wa Wimbo wa Taifa ukipigwa katika ukumbi wa
Mlimani City kabla ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan alipohutubia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Sehemu ya Wazee wa Mkoa wa
Dar es Salaam waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mkutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021PICHA NA IKULU
Social Plugin