Bw. Ngusa Dismas Samike
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa baadhi ya makatibu tawala wa mikoa, kuwahamisha baadhi na wengine kuwabakiza kwenye vituo vyao vya kazi. Lakini pia amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa taasisi. Miongoni mwa walioteuliwa ni aliyekuwa Katibu wa Rais Ikulu Bw. Ngusa Dismas Samike ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Rais Samia pia amemteua aliyekuwa Afisa Katika Ofisi ya Rais Bw. Mussa Ramadhan Chogello kuwa katibu Tawala Mkoa wa Geita.
Uteuzi huo umeanza Mei 29,2021 na wataapishwa Juni 2,2021 saa 4 asubuhi Ikulu Chamwino Dodoma
Social Plugin