Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI WAJIPANGA KUIMARISHA USALAMA MTANANGE SIMBA SC Vs YANGA


Kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limejipanga kuimarisha usalama katika mechi ya Watani wa Jadi Simba dhidi ya Yanga Mei 8, 2021 katika Dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa ametoa rai kwa wazazi wanaopenda kwenda na Watoto uwanjani kuwa makini na kutoruhusu Watoto kuzagaa uwanjani na kupelelea kupotea.

Katika hatua nyingine amewataka mashabiki na wapenzi wa vilabu hivyo kutokuwa chanzo cha uvunjifu wa amani katika mchezo huo na endapo watakiuka sheria hawatosita kuwawajibisha.

“Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha usalama katika mtanange huo wa watani wa jadi, tunasisitiza utulivu na kutovunjwa kwa sheria kwakuwa tutakuwa kazini hatutosita kuchukua hatua kwa yeyote atakayekuwa na viashiria vya kuvuruga utaratibu na sheria”, amesema Kamanda Mambosasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com