Hatimaye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeweka wazi taarifa rasmi kuhusu sakata la kuahirishwa kwa mechi namba 208 ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kati ya Watani wa Jadi Simba na Yanga iliyotakiwa kuchezwa Mei 8 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, amezitaka mamlaka za serikali zinazohusika na masuala ya tiketi kuhakikisha zinawapatia tiketi upya mashabiki takribani 43,000 waliokuwa wamekata tiketi.
Aidha ameagiza mamlaka za soka ikiwemo Bodi ya Ligi na TFF, kupanga upya tarehe ya mechi ya Simba SC vs Yanga.
Social Plugin