AFRIKA KUSINI YAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUFUGA SIMBA NYUMBANI



Afrika kusini imeweka wazi mpango wa kuzuia watu kuwazalisha simba majumbani kwa lengo la kuwahifadhi kama wanyama wa nyumbani, kuwavutia watalii ama kuwindwa.

Hatua hiyo imejiri baada ya kuchapishwa kwa matokeo ya uchunguzi wa miaka miwili kuhusu mtindo wenye utata wa baadhi ya watu kuendeleza uzalishaji wa simba ambao wamezuia katika mbuga za binafsi na majumbani.

Iligundulika kwamba mtindo huo ulihatarisha juhudi za uhifadhi wa wanyama hao na pia madhara kwa wafugaji.

Serikali ya Afrika Kusini imekubali mapendekezo ya jopo lililofanya uchunguzi huo hatua ambayo huenda haitawafurahisha wadau katika sekta ya uwindaji.

" Ripoti hiyo inapendekeza kupigwa marufuku kwa mipango ya kuzalisha simba au kuwaweka majumbani ' waziri wa Mazingira Barbara Creecy amesema .

"Hatutaki kuzalishwa"

 Via BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post