Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. YONAZI : SERIKALI IPO TAYARI KUFANYIA KAZI MAONI YA WADAU WA SEKTA NDOGO YA UTANGAZAJI


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jimmy Yonazi akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa kufungua kikao cha Majadiriano ya Jinsi ya Kuboresha Huduma za Utangazaji uliofanyika jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari akitoa maeleylzo kuhusiana na Sekta ya utangazaji katika kikao cha Majadiriano ya Jinsi ya Kuboresha Sekta ya Utangazaji ,kilichofanyika jijni Dar es Salaam.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Habari Dkt.Jimmy Yonazi akisikiliza maoni ya wadau katika kikao cha majadiriano ya jinsi kuboresha Sekta ya Utangazaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi akiwa picha ya Pamoja na wadau Mara baada ya kufanyika kikao cha majadiriano ya jinsi kuboresha huduma ya Sekta ya Utangazaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

*****************************

Na Mwandishi Wetu

Serikali imeahidi kufanyia kazi maoni ya uboreshaji wa huduma za Utangazaji yaliyotolewa na wadau katika kikao cha mashauriano ya jinsi ya kuboresha huduma za Utangazaji nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar es salaam, ambacho kiliunganisha wadau kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jimmy Yonazi amesema Serikali iko tayari kujifunza kutoka kwa wadau hivyo washiriki wawe huru katika kuchangia.

Kikao hicho ambacho kimeratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kimekusanya maoni katika maeneo matano ambayo ni pamoja na tozo za leseni za Redio, Televisheni, Maudhui mtandaoni na Masafa ya Utangazaji.

Maeneo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na mfumo wa biashara kwenye urushaji wa matangazo ya televisheni yanayorushwa bila kulipia na mfumo wa biashara kwenye matangazo ya televisheni ya kulipia.

Aidha, matumizi ya kisimbusi kimoja ili kupata maudhui kutoka kwa watoa huduma tofauti; mikataba ya kibiashara kati ya vituo vya utangazaji na wasambazaji wa matangazo; na wajibu wa vituo hivyo katika leseni pia vimejadilidiwa.

Hii ni mara ya sita kwa mwaka huu 2021 ambapo TCRA imekuwa ikiandaa mikutano ili kubadilishana mawazo na uzoefu kwa lengo la kuboresha huduma za Mawasiliano.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com