Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives mkoani Shinyanga Jonathan Manyama, akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Stadi za Maisha kwa walimu wa Shule ya Msingi Shilabela na shule y Sekondari Pandagichiza wilayani Shinyanga kupitia mradi wa Shule salama kwa wote.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Shirika la Thubutu Africa Initiatives la mkoani Shinyanga, ambalo linatetea haki za wanawake na watoto, limefunga rasmi mafunzo ya Stadi za maisha shuleni, kwa walimu katika kata ya Pandagichiza wilayani Shinyanga.
Mafunzo hayo yameshirikisha walimu 19 kutoka katika shule ya msingi Shilabela na shule ya sekondari Pandagichiza wilayani Shinyanga, ambayo ni sehemu ya mradi wa Shule Salama kwa wote unaofadhiliwa na mfuko ruzuku wa wanawake Women Fund Tanzania (WFT).
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo leo mgeni Rasmi Bi. Glory Mbia ambaye ni mratibu wa mfuko wa ruzuku wanawake Women Fund Tanzania mkoani Shinyanga, amewataka walimu kuyatumia mafunzo hayo vizuri katika makuzi ya wanafunzi shuleni.
"Nalipongeza sana Shirika hili la Thubutu kwa kazi nzuri ambayo mmeifanya, nawapenda sana walimu sababu nawapenda watoto, na walimu ndio wanalinda ustawi wa mtoto, na watoto ndiyo Taifa la kesho, hivyo mradi huu umelenga penyewe," alisema Mbia.
Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo la Thubutu Africa Initiatives Bw. Jonathan Manyama Kifunda, alisema mafunzo yaliyotolewa kwa walimu hao ni Stadi za maisha, ili kufanya Shule kuwa mahali salama kwa watoto wote, ambapo pia wamepewa elimu ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia.
Alisema walimu hao 19 wameiva katika mafunzo hayo, na watakuwa waelimishaji wazuri wa Stadi za maisha kwa wenzao pamoja na wanafunzi na jamii, ambapo pia wamepewa mbinu za ziada za ufundishaji bora, ili wanafunzi waelewe masomo yao na kupata ufaulu mzuri.
Naye Mwalimu Elifaraja Josephat, akisoma risala kwa niaba ya walimu hao, alisema mafunzo hayo yalianza February 9 mwaka huu, na yamekamilika April 30, na kuahidi kuyatumia vyema katika kazi zao za ufundishaji.
Alisema mafunzo hayo ya Stadi za maisha, pia yamewaongezea maarifa na ujuzi, pamoja na kuboresha nidhamu kwa wanafunzi, sababu wamekuwa wakiwapatia elimu hiyo.
"Elimu hii imeleta mabadiliko chanya katika maisha yatu, na ufundishaji, ambapo imepandwa katika udongo mzuri wenye rutuba, na itafanya vizuri na kustawi vyema" alisema Josephat.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Pandagichiza George Chapenemecho , alipongeza mafunzo hayo kutolewa kwa walimu shuleni hapo, yamesaidia kwa kiasi kikubwa kubadili mfumo wa maisha ya walimu na wanafunzi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mratibu wa Mfuko wa ruzuku wanawake Women Fund Tanzania (WFT) mkoani Shinyanga Glory Mbia ambaye alikuwa mgeni Rasmi akizungumza kwenye hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo ya Stadi za Maisha shuleni kwa walimu Pandagichiza.
Glory akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Manyama, akizunguza kwenye hafla hiyo.
Afisa elimu Kata ya Pandagichiza Irene Ringo, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kufunga mradi wa Stadi za Maisha shuleni kwa walimu.
Meneja miradi kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiatives Paschalia Mbungani akizungumza kwenye hafla hiyo ya kufunga mradi.
Mwalimu Elifaraja Josephat, akisoma Risala kwa niaba ya walimu wenzake, ambao wamepata mafunzo ya Stadi za Maisha Shuleni.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Pandagichiza George Chapenemecho, akitoa shukrani kwenye hafla hiyo ya kufunga mradi.
Mwalimu Mzugulu Mchulo wa Shule ya Sekondari Pandagichiza, akitoa ushuhuda namna mafunzo hayo ya Stadi za Maisha Shuleni yalivyombadili.
Mwalimu Felton Kisabo akitoa ushuhuda namna mafunzo hayo ya Stadi za Maisha Shuleni yalivyombadili.
Walimu wa Shule ya Msingi Shilabela na Sekondari ya Pandagichiza wakiwa kwenye hafla ya kufunga mafunzo yao ya Stadi za Maisha Shuleni.
Walimu wakiwa kwenye hafla ya ufungaji wa mafunzo.
Walimu wakiwa kwenye hafla ya ufungaji wa mafunzo.
Walimu wakiwa kwenye hafla ya ufungaji wa mafunzo.
Mgeni Rasmi Mratibu wa mfuko wa ruzuku wanawake Women Fund Tanzania mkoani Shinyanga Grory Mbia, kulia akigawa cheti kwa Mwalimu ambaye amehitimu mafunzo ya Stadi za Maisha Shuleni.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Walimu wakimlisha Keki Mgeni Rasmi, katika Hafla hiyo Mratibu wa mfuko wa ruzuku wanawake Women Fund Tanzania mkoani Shinyanga Grory Mbia.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Afrika Intiatives, Jonathan Manyama, akila keki kutoka kwa walimu katika hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo ya Stadi za Maisha Shuleni.
Picha ya Pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika hafla ya kufunga mafunzo ya Stadi za Maisha Shuleni kwa Walimu wa Pandagichiza wilayani Shinyanga.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Social Plugin