Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PASTA ATOZWA FIDIA YA KONDOO BAADA YA KUFUMANIWA AKICHEPUKA NA MKE WA MTU...WAZEE WASIMAMIA TALAKA

Pasta wa Kanisa la African Divine eneo la Lugari, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya ambaye alifumaniwa akifanya ngono na mke wa muumini wake amepigwa ya KSh2,000 sawa na shilingi 42,000 ya Tanzania.

Mhubiri huyo aliyetambuliwa kwa jina Samuel pia alitozwa faini ya ng'ombe na kondoo kama adhabu kutoka kwa baraza la wazee wa jamii ya Kabras kutokana na kuhondomola mke wa mtu.

Samuel alipatikana na hatia ya kuchovya asali ya mke wa Charles Mulongo kwenye kitanda chao cha ndoa katika kijiji cha Mufutu siku ya Ijumaa, Mei 7,2021.

Kulingana na wazee hao, pesa hizo zitatumika katika kutakasa boma la Mulongo ili kuzuia familia yake dhidi ya mapepo ya usherati.

 Wazee hao pia waliidhinisha talaka kati ya Mulongo na mkewe aliyekiri kuwa alifurahia uwezo wa mhubiri huyo kitandani baada ya mume wake kumtelekeza.

Mulongo alikuwa amemtembelea mkewe wa tatu ambapo alitarajia kulala usiku huo Alhamisi, Mei 7,2021 alipopokea habari kwamba wanawe walikuwa wamempata mtu wasiyemjua katika chumba chake cha kulala. 

"Nilikuwa katika nyumba yangu nyingine wakati nilipigiwa simu na mmoja wa majirani akinijulisha kuwa kuna mtu ameshikwa akiwa na mke wangu. Mwanamke hapaswi kukudharau kwa kiwango ambacho analeta wanaume chumbani kwako. Siwezi kuvumilia suala kama hilo," alisema. 

Mulongo alisema kuwa ni kitendo ambacho hakukitarajia kwa kuwa alikuwa anaheshimu pasta Samuel ambaye amekuwa akitoa mahubiri moto moto kanisani. 

Tukio hilo linajiri wiki mbili baada ya Askofu mstaafu wa Kanisa la Kianglikana Uganda, Stanley Ntagali, kuomba msamaha hadharani kwa kushiriki mapenzi na mke wa mtu.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com