CP Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) mteule
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amempandisha cheo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Camilius Wambura, na kuwa Kamishna wa Polisi (CP) ambapo pia amemteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kueleza kuwa uteuzi huo umeanza jana Mei 30, 2021.
Mei 17, 2021, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha Wambura kutoka kuwa 'Chief of Operations Upel' kuu Dodoma na kumhamishia Dar es Salaam kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum akichukua nafasi ya SACP Lazaro Mambosasa.