Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA : WATOTO TUNZENI WAZEE



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka jamii kutunza wazee huku akiwasisitiza watoto kutunza wazee wao.

Rais Samia ameyasema hayo leo Ijumaa Mei 7,2021 wakati akizungumza na wazee wa Dar es salaam

"Watoto tunzeni wazee, awe mzee wako au siyo mzee wako mtunze. Awe ni mzee wa ukoo ni wajibu wako kutunza. Tutunze wazee wetu ndani ya familia zetu licha ya kwamba serikali inaendelea kujenga na kuboresha makazi ya wazee",amesema Rais Samia

"Makazi ya Wazee Kolandoto Shinyanga tumeyafanyia marekebisho makubwa na wazee wanaishi vizuri.Tutaendelea kujenga makazi ya wazee katika maeneo mengine",ameongeza.

Rais Samia amesisita umuhimu wa kuwapa heshima wazee huku akiwasisitiza vijana kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kuwapisha wazee wakae kwenye vyombo vya usafiri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com