COSOTA YAWASISITIZA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI KUWA NA UMOJA
الاثنين, مايو 03, 2021
Na Anitha Jonas – COSOTA,Dar es Salaam
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki COSOTA Doreen Anthony Sinare amewataka waimbaji wa nyimbo za Injili kuwa na Umoja kwa kuwa kuanzisha Shirikisho litakalowaunganisha vyema.
Doreen ameyazungumza hayo Mei 02, 2021 katika Kipindi cha Super Sunday kilichokuwa kinarushwa na Boresha Online Redio ambapo kilikuwa na Mada inayosema ni kwa namna gani COSOTA inafanya kazi na waimbaji wa Injili pamoja na faida za kusajili kazi COSOTA.
Akiendelea kuzungumza katika kipindi hicho Mtendaji huyo ambaye ni Msimamizi wa Hakimiliki nchini alieleza kuwa Serikali inatambua changamoto ya ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu masuala ya Hakimiliki hivyo imeanza kuandaa vipindi vya kutoa elimu na kwa mwaka mpya wa fedha 2021/2022 kutakuwa na Mfuko wa Sanaa na Utamaduni ambao utasaidia kutoa elimu na mikopo kwa wasanii.
“Kufuatia changamoto kubwa ya uuzaji na usambazaji wa kazi Sanaa Serikali imeandaa mfumo wa Online ambao utasaidia kusambaza kazi hizo ikiwemo Muziki, Filamu na kazi zingine za Sanaa,”alisema Doreen.
Pamoja na hayo Doreen alizungumzia suala la ugawaji wa Mirabaha kwa kuelezea changamoto ya ukusanyaji wa mirabaha kutokana na uhaba wa watumishi, ambapo alifafanua kuwa kuanzia mwakani COSOTA itaanza kutoa gawio kubwa baada kufanya marekebisho ya Kanuni mbalimbali na kuboresha mifumo ya ukusanyaji.
Akijibu hoja ya Mmoja wa Waimbaji wa Kikundi cha Zablon Singers kuhusu kurudiwa kwa wimbo wa mtu bila ridhaa ya mwenye wimbo Doreen alisisitiza kuwa hilo ni kosa katika suala la Hakimiliki, hivyo aliendelea kutoa Onyo kali kwa Wasanii kuacha mara moja tabia hiyo kwani hiyo ni kinyume na taratibu za Hakimiliki.
Halikadhalika nae Mtangazaji wa Kipindi hicho Mc Mtawala aliiomba COSOTA kutoa elimu kwa Makanisa ya Kikristo ambayo yanakataza kwaya zao kusajili nyimbo zao kwa ajili ya kupata Hakimiliki
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin