Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BINTI AMUUA KAKA YAKE AKIKOMAA PESA YA CHAKULA AITUMIE KUSUKA NYWELE


Wakazi wa kijiji cha Kibichoi katika kaunti ya Kiambu nchini Kenya wameachwa vinywa wazi baada ya msichana mwenye umri wa miaka 15 kumuua kaka yake Antony Nganga, kabla ya kutoroka.

Chanzo cha mauaji hayo ni KSh 200 ambazo ni sawa na shilingi 4,200 za Tanzania ambazo mama yao aliwaachia kununua chakula.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), awili hao walitofautiana kuhusu namna watagawana pesa hizo huku msichana akitaka kutumia pesa hizo kusuka nywele.

"Msichana huyo alitaka pesa hizo atengeneze nywele badala ya kununua chakula lakini kaka yake mkubwa alikataaa kumsikiliza," ilisema idara hiyo kama ilivyonukuliwa na TV47.

Tofauti zao zilimpelekea msichana huyo kumjeruhi kaka yake mkubwa mwenye umri wa miaka 18 akitumia kifaa cha jikoni na kumuacha akiwa amepoteza fahamu.

Kisha mwathiriwa alikimbizwa katika Hospitali ya Kigumo Level Four na mjomba wake John Wangendo, ambapo alithibitishwa kufariki dunia walipowasili.

Makachero wa DCI wameanzisha msako wa msichana huyo.

CHANZO- TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com