DC SELELA: UNAWEZA KWENDA SEHEMU USIONE CHANGAMOTO LAKINI JICHO LA MWANAHABARI LINAMULIKA KILA MAHALI NA KUONESHA NJIA



Mkuu Wilaya ya Kongwa Dkt. Suleiman Serera (katikati) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akimkabidhi tuzo Afisa Uhusiano wa TANESCO mkoa wa Dodoma Innocent Lupenza ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika ukumbi wa Jiji (Madiwani) jijini Dodoma. Tuzo hiyo imetolewa leo na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) kutambua mchango wa Bw Lupenza katika tasnia ya habari.CPC imeanzisha tuzo hizo ili kutambua mchango wa wadau mbalimbali wanaotoa ushirikiano,na kufanikisha waandishi kutimiza majukumu yao.
Wadau wa Habari wakiwa katika maadhimisho ya Uhuru wa Habari duniani kwa Mkoa wa Dodoma yakiadhimishwa Mei 8,2021
***
Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Seleman Selela  amesema  tasnia ya Habari ina mchango mkubwa katika kuibua changamoto za jamii ili kuweza kutatuliwa na serikali.

Mkuu huyo wa wilaya amebainisha hayo leo Mei 8,2021  katika maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya Habari mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Klabu ya  Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma[CPC] kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania [UTPC],Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa[TANAPA]pamoja na mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma[DUWASA].

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ,mkuu huyo wa wilaya amesema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi  huku pia akiwataka wanahabari kuendelea kuwa na ubunifu katika uchakataji wa habari.

Katika hatua nyingine Selela amewataka wanahabari kwendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kuhakikisha wanaandika habari zenye mizania[balance]ili kuweza kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.

Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa  Dodoma [CPC]Musa Yusuph ameainisha changamoto zilizopo katika tasnia ya   habari ni pamoja na ubaguzi wa baadhi ya taasisi za serikali kuita vyombo vya habari kuelezea mambo nyeti ya kitaifa huku Katibu wa klabu hiyo Ben Bago akiwaasa baadhi ya maafisa habari serikalini kuacha tabia ya  kutoa lugha isiyokuwa na staha kwa wanahabari pindi wanapotekeleza majukumu yao.

Afisa Mhifadhi mkuu Mamlaka ya Hifadhi Tanzania[TANAPA]Jully Lyimo pamoja afisa utalii mkoa wa Manyara Cecilia Mkwabi wamelezea mchango wa Habari katika sekta ya utalii nchini.

Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yalifanyika Mei 3,2021  ambapo mkoa wa Dodoma yakifanyika Mei,8,2021 yakienda sambamba na kaulimbiu isemayo Habari kwa maufaa ya umma  ambapo tuzo zimetolewa kwa taasisi zilizo na ushirikiano mkubwa kwa tasnia ya Habari kuwa ni TANAPA  na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma [DUWASA  na Mwanachama bora wa mwaka akiwa ni Sebastian Warioba huku tuzo iliyokwenda kwa afisa habari mwenye ushirikiano mzuri ni Innocent Lupenza kutoka TANESCO.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post