Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT FLORENCE SAMIZI (CCM) ASHINDA UBUNGE JIMBO LA MUHAMBWE


Mgombea wa CCM, Dkt. Florence Samizi ameibuka mshindi uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Muhambwe. Awali, jimbo hili lilikuwa likiwakilishwa na marehemu Mhandisi Atashasta Nditiye.

Dkt. Samizi ameshinda uchaguzi huo baada ya kupata kura 23,441 kati ya kura 35,339 sawa na asilimia 68 akifuatiwa na Mgombea wa Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Bw. Masabo Julius aliyepata kura 10,847 na Mgombea wa Democratic Party (DP), Bw. Philipo Fumbo aliyepata kura 368.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com