Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PASTA ANASWA 'LIVE KITANDANI' AKIPAKUA ASALI YA MKE WA MTU


Wakazi wa kijiji cha Mufutu huko Lugari, kaunti ya Kakamega nchini Kenya wameshuhudia kisanga baada kumfumania Mchungaji wa Kanisa la African Divine aliyejulikana kwa jina moja la Samwel akiwa uchi wa mnyama katika chumba cha kulala akipakua asali ya mke wa kwanza wa Charles Mulongo.

Inaelezwa kuwa Mulongo alikuwa amemtembelea mkewe wa tatu ambapo alitarajia kulala usiku huo Alhamisi, Mei 7,2021 alipopokea habari kwamba wanawe walikuwa wamempata mtu wasiyemjua katika chumba chake cha kulala. 

"Nilikuwa katika nyumba yangu nyingine wakati nilipigiwa simu na mmoja wa majirani akinijulisha kuwa kuna mtu ameshikwa akiwa na mke wangu. Mwanamke hapaswi kukudharau kwa kiwango ambacho analeta wanaume chumbani kwako. Siwezi kuvumilia suala kama hilo," alisema.

Baada ya kutanabahi kwamba tabia zake zilikuwa zimefichuka, Mchungaji/Pasta alianza kukabiliana na kifungua mimba wa kiume wa Mulongo.

 "Nilipofungua mlango, nilimkuta akiwa uchi kitandani. Alijaribu kupigana nami lakini nilifanikiwa kumshika. Aligundua kuwa arobaini zake zilikuwa zimefika, akaruka kutoka chumbani na kutoweka gizani," mmoja wa wana wa Mulongo alisimulia.

 Wakazi hao sasa wanapanga kufanya tambiko ili kusafisha nyumba ya Mulongo kulingana na mila ya Kabras kufuatia tukio hilo.

Karibu wiki mbili zilizopita, Askofu mstaafu wa Kanisa la Kianglikana Uganda, Stanley Ntagali, aliomba msamaha hadharani kwa kushiriki mapenzi na mke wa mtu. Mchungaji huo alikiri kufanya mapenzi na Judith mbele ya maaskofu wa Kianglikana na makuhani waliokusanyika katika Kanisa Kuu la Namirembe kusherehekea miaka 60 tangu kanisa hilo lianze kujitawala mnamo Jumanne, Aprili 27.

"Ndugu zangu maaskofu, washirika wetu wote, ndugu na dada, kanisa lote la Uganda na washirika wetu wote ulimwenguni kote na familia ya Mch Christopher mkewe Judith, familia hizo mbili naomba mnisamehe. Na ninataka kubaki karibu na Yesu, "Ntagali aliomba.

CHANZO - TUKO NEWS


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com