Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu,ACP Richard Abwao
**
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Edward Manyangu (41) mkazi wa kijiji cha Ijitu wilaya ya Busega mkoani Simiyu anadaiwa kumuua mkewe Dalali Maunga (41) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani akimtuhumu kugawa asali ya ndoa kwa mwanaume mwingine.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Mei 11,2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea Mei 10, 2021 baada ya wana ndoa hao kuingia kwenye mvutano kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine nje ya ndoa.
"Kwa mujibu wa ujumbe wa maandishi unaoaminika kuandikwa na kuachwa na Manyangu, alikuwa akimthumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.Baada ya kufanya mauaji hayo naye alijiua kwa kujinyonga kwa kamba aliyofunga juu ya mti ulioko nje ya nyumba yao",amesema Kamanda Abwao.
Social Plugin