Mahakama ya Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es salaam imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elisha Mushi (22), mkazi wa Ubungo Kibangu baada ya kuthibitika kumlawiti mtoto wa miaka minne kanisani.
Mushi, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kufundisha watoto kanisani anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 19, mwaka huu katika Kanisa la Embassy Kingdom.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ester alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa, mahakama imejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa analotuhumiwa nalo.
Via Mwananchi
Social Plugin