Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHUHUDIA MAAJABU YA NG'OMBE WANAOOGELEA KAMA BINADAMU


Ng'ombe wakiogelea na binadamu
Jamii ya Njemps au Ilchamus

Mwandishi ni Kevin Anindo, Kaunti ya Nairobi.

Hii ni Afrika na Afrika kuna mengi ya kuvutia. Leo nakuangushia makala kuhusu mila ya zamani ya kabila la eneo la Ziwa Baringo linalohusishwa na biashara na maisha ya kabila lililo katika hatari ya kuangamia inakuwa kivutio halisi cha watalii, hasa kipindi hiki Kenya inapoendelea kushuhudia kuimarika zaidi kwa utalii wa ndani na kupungua kwa wageni au kusafiri nje kwa matajiri.

 Hili ni tukio la "ajabu" lisicho la kawaida la ng'ombe wanaoogelea wa Kisiwa cha Kokwa. Jamii ya wafugaji ya Njemps, kabila la dogo la Wamaasai ambalo idadi ya watu wake ni zaidi ya 30,000, hawana njia nyingine ya kuuza ng'ombe wao zaidi ya kusafirisha kila wiki kwenda sokoni katika mji wa Marigat.

Njemps ni moja ya jamii zinazotajwa kuwa maskini sana na wana mitumbwi ya miti ya asili ambayo hawawezi kuitumia kusafirishia ng'ombe wao hadi okoni, kwa hivyo kwa miaka mingi wamefundisha ng'ombe wao kuogelea kwenye maji ya ziwa kufikia ufukweni kutoka kisiwa hicho.

 Kwa muda baada ya hamu ya kushuhudia ng'ombe hao wakiogelea, tukio hilo sasa ni moja katika vivutio vya utalii huko Baringo na eneo jirani na mara nyingi ng'ombe hao husindikizwa na boti zilizobeba watalii na wao hufurahia kupiga picha na video hata kwa kutumia simu zao za rununu. 

Wakati mwingine, boti zile zile ambazo, kwa upande mwingine, labda zinamilikiwa na hoteli ambazo hutumika kushuhudia "kivutio hicho cha kabila hili" hutumiwa kuwabeba ng'ombe hao. 

Lakini ni vipi ng’ombe wanaojulikana kuwa waoga wa maji ya kina kirefu hufaulu kuogelea?

 Ingawa ng'ombe kwa kawaida ni mwogeleaji mzuri lakini inategemea mazingira, anaweza kuogelea vizuri-kama sio bora-kushinda mwanadamu. Maeneo mengine mfano hili tunalozungumzia, ng'ombe huogelea kwenye maji ya vina tofauti na ni sehemu ya maisha yao.

Mmoja wa wafugaji wa eneo hilo aliyezungumza na TUKO.co.ke alisema, "Walishaji mifugo wa Njemps hupeleka mifugo wao hadi kwenye ufukwe wa kisiwa hicho, kisha huwatupa majini ndama lakini wakiwa makini wasije wakazama au kusombwa.

"Kwa kuhofia kumpoteza ndama ng'ombe hufuata ili kuwaokoa na polepole watajifunza kuogelea.Wao huwarejesha ndama wao ufukweni na kisha tukio hilo hurejelewa mara kadha kwa kipindi fulani, mpaka watakapozoea kuogelea peke yao, bila kujali sana kuokoa watoto wao". 

Mazoea huwafanya ng'ombe kuwa tayari muda wote kuvuka mito peke yao kwa msaada mdogo. Lakini ni bora kufahamu kuwa, haimaanishi ng'ombe wanaoogolea wanaweza kuogelea tu bila kikomo.

 Ng'ombe wakianguka kwenye maji, wanahitaji njia ya kuwawezesha kutoka nje kabla ya kuchoka na labda kuzama. Nyakati nyingi, mito na maziwa huwa na maeneo yanayoteremkia fukweni ambayo huwasaidia ng,ombe walioingia kwenye maji hayo kutoka nje salama.

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com