Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho anatarajia kuwaapisha Majaji 28 wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu aliowateua siku chache zilizopita.
Taarifa iliyotolewa leo na kusambazwa kwenye vyombo vya habari na , Mkurugenzi wa kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa imebainishwa kuwa hafla ya kuwaapisha majaji hayo itafanyika kuanzia saa tatu asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Kikwete.
Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa keshokutwa Rais Samia atawapisha wakuu wa mikoa na wakuu wa taasisi aliyowateua Mei 15, 2021.
Social Plugin