Na Faustine Gimu,Dodoma
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma Mlezi wa Mashindano hayo ya Miss Dodoma na Morogoro ambaye pia ni Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Morogoro Norah Waziri Mzeru amesema kuwa jamii itambue Tasnia ya Urembo na Mitindo imekuwa chachu katika kujengewa mabinti uwezo wa kijasiriamali,kijamii na kiutamaduni.
Aidha,Mhe.Mzeru amewaomba viongozi mbalimbali na Taasisi binafsi na za kiserikali hususan wabunge na wafanyabiashara kuwasaidia mabinti katika tasnia ya urembo na mitindo kuwapatia michango mbalimbali ili kuweza kuendeleza Tasnia ya urembo Nchini.
"Nikiwa kama mbunge wa viti maalumu mkoa wa morogoro katika Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania nawaomba wabunge wenzangu kuchangia Tasnia ya urembo na Mitindo kwani inatoa Ajira kwa mabinti zetu pamoja na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji nchini",amesema .
Kwa upande wake mkurugenzi wa NIKALEX LTD Alexander Nikitas ambae pia ni mwandaaji wa mashindano hayo amesema kuwa hii ni fursa kwa mabinti wa mkoa wa dodoma kujitokeza kwa wingi ili kushiriki mashindano haya ambayo yatawapa nafasi za kushiriki Miss Tanzania na mshindi wa kwanza mpaka wa tatu ndiye atakayepata nafasi ya kushiriki Miss Tanzania.
"Kabla ya Mashindano haya kufanyika ,Tarehe 21 mwezi wa 6 mwaka huu tutawakutanisha washiriki na yatahusisha wilaya zote saba za Dodoma hivyo mabinti wote mnakaribishwa kushiriki mashindano haya"amesema Nikitas
Pia Nikitas amesema jamii itambue kuwa tasnia ya urembo na mitindo imekuwa chachu katika kuwajengea mabinti kuwa wana jamii wenye kutegemewa wawapo katika mashindano haya.
Afisa Habari wa Mashindano hayo Ezekiel Kwakwa amewahakikishia Wanadodoma na watanzania kwa ujumla kuwa mashindano hayo yatakuwa ya haki na vigezo vyote vitazingatiwa na hakutakuwa na upendeleo wowote.
" Katika mashindano haya haki itatendeka hakuna upendeleo wowote utakaojitokeza"amesemaKwakwa.
Mashindano hayo yameshirikisha Warembo kutoka vyuo mbalimbali mkoani Dodoma na usaili unaendelea katika wilaya zote za Dodoma.
Mashindano ya Miss Dodoma yatahitimishwa Rasmi mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu.
Social Plugin