MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia
Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia
Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira amesema ipo haja ya Serikali
kuanzisha Mahakama ya Familia yaani Family Court kama ilivyofanya kwenye
Mahakama za Ardhi ili kusaidia kuondosha changamoto zinazojitokeza
ikiwemo Masuala ya Matunzo ya Watoto.
Amesema
ili Matunzo ya Watoto yaweze kubebwa kwa uzito unaostahili na kupanua
wigo mpana wa haki ili kuhakikisha changamoto za namna hiyo zinaondoka
kwenye jamii badala ya kuendelea kuwepo kila wakati.
Aliyasema
hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati alipouliza Maswali Mawili ya
Nyongeza baada ya Serikali kuwasilisha Majibu ua Swali lake la Msingi
lililouliza "Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwakomboa Wanawake
wanaobebeshwa mzigo mkubwa wa kugharamia matunzo ya Watoto bila msaada
wa Baba?"
Mbunge Neema
alisema pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini hata kwa Sheria
zilizopo bado kuna changamoto kubwa kwenye eneo hilo.
Mbunge
Neema Lugangira alisema ndio maana hata Chama cha Mapinduzi (CCM)
kwenye Ilani yake ya Uchaguzi 2020/2025 imeliona hilo na imeahidi
kuielekeza Serikali kwenye Ukarasa wake wa 145 unaosema "CCM itaelekeza
Serikali kuimarisha huduma za usuluhuhi wa migogoro ya ndoa na matunzo
kwa watoto" na kwa msingi huo aliuliza maswali yake mawili ya nyongeza.
Katika
maswali yake ya nyongeza Mbunge Lugangira aliishauri Serikali iboreshe
Sheria zilizopo ili gharama za matunzo ya watoto iendani na hali ya
uchumi wa sasa na maisha ya sasa kutokana na maisha kuwa juu kuliko
ilivyokuwa awali.
Akijibu
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Mhe Mwanaidi
Khamisi amesema "Serikali imetoa maelekezo wazazi kuhakikisha mtoto
anapata matunzo yote stahiki, na kama wazazi wa mtoto hawaishi pamoja na
mtoto anaishi na Mama yake basi Baba atawajibika kugharamia malezi ya
mtoto kulingana na kipato alichonacho". Swali hili pia lilimnyanyua Mhe
Waziri Dkt Dorothy Gwajima ambae alisema "Nakiri tatizo Watoto
kutelekezwa ni kubwa na ipo haja ya Serikali kufanya harakati za ziada
ili kulidhibiti.
Kwa
upande mwingine Mbunge Neema Lugangira aliishauri Serikali ianzishe
Mahakama ya Familia yaani Family Court na kwa upande wa Serikali, Mhe
Naibu Waziri Mwanaidi Ali Khamis alisema Serikali imekubaliana na
ushauri wa Mbunge Neema Lugangira na ipo haja ya kuwa na chombo maalumu
ambacho kitakuwa kinashughulikia masuala la familia hivyo wameupokea
ushauri wa Mbunge Lugangira na wataufanyia kazi kulingana na Sheria
zilizopo.