Mamia ya wakazi wa Shinyanga na mikoa jirani wamejitokeza
kwenye mazishi ya Mshereheshaji Maarufu MC Dickson Mitundwa (27) katika Makaburi ya Old Shinyanga katika Manispaa ya
Shinyanga leo Alhamis Mei 13,2021.
MC Dickson Mitundwa alifariki dunia Mei 10,2021 jijini Dar es salaam baada ya kuugua ghafla akiwa Hotelini akijiandaa na safari ya kurejea nyumbani kwao mkoani Shinyanga ambapo alikimbizwa kituo cha afya Palestina Sinza kwa ajili ya matibabu na kuthibitika kuwa amefariki dunia.
Soma pia :👉 Tanzia : MC DICKSON MITUNDWA AFARIKI DUNIA
MC Dickson Mitundwa ameacha mke mmoja.
PICHA ZOTE NA WILCAN
Mc Dickson Mitundwa enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Dickson Mitundwa leo Alhamis Mei 13,2021 . Picha zote na Wilcan
Social Plugin