Waendesha bodaboda wa kituo cha Kisangiro kata ya Kilema Kaskazini wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wamevamia msiba wa Lenard Abel (20) na kumwaga chakula na pombe kwa madai kuwa marehemu alikuwa hapewi chakula alipokuwa hai.
Shuhuda wa tukio hilo, Lucy Lyimo amesema kundi hilo la vijana lilifika msibani na kuvamia jikoni na kuanza kumwaga chakula na pombe aina ya mbege sambamba na kuvunja viti.
“Wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula kulitokea kundi la vijana zaidi ya ishirini wakipiga ukunga na kusema huyu marehemu kipindi akiwa hai alikuwa hapewi chakula iweje leo amekufa chakula kipo na pombe, " amesema Lucy akibainisha wakati wakisema hayo walikuwa wakielekea ilipohifadhiwa pombe na chakula
Via Mwananchi
Social Plugin