Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PROF.MKENDA : SERIKALI KUWEKA KIPAUMBELE CHA KWANZA KUFANYA UTAFITI WA MBEGU ZAO LA MUHOGO ILI KUONGEZA UZALISHAJI


Waziri wa kilimo Prof.Adolf Nkenda


Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma


Serikali imesema itaweka kipaumbele cha kwanza kufanya utafiti wa mbegu zao la muhogo ili kuongeza uzalishaji kutoka tani 8 hadi tani 50 kwa hekta.

Hayo yamebainishwa Leo Mei 7,2021 jijini Dodoma na Waziri wa kilimo Prof.Adolf Nkenda katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kilimo Tanzania wenye lengo la kuongeza tija na kutumia fursa za masoko kwa zao hilo.

Prof. Mkenda ameainisha mikakati kabambe katika kuongeza tija zao la muhogo kuwa ni pamoja na uzalishaji kwa wingi na kuongeza bajeti.

Aidha Prof.Mkenda ameagiza kila afisa ugani anakuwa na shamba darasa kuanzia ekari moja na kuendelea .

Katika hatua nyingine Prof. Mkenda amesema maafisa ugani wote watanunuliwa simu za mkononi na kuunganisha na mfumo wa Mobile kilimo hali itakayorahisisha kujua kanzi data wanafanya nini kwa siku.

Pia Waziri huyo wa kilimo amesema serikali itahakikisha inaimarisha masoko ya zao la muhogo huku akitumia fursa hiyo kuipongeza Wilaya ya Kahama kwa kuendelea kufanya vizuri kwa vyama vya ushirika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo Nyasebwa Chimago amebainisha malengo mengine ya Mkutano huo ni kutambua changamoto za zao la muhogo na kuzindua mikakati wa miaka 10 wa zao hilo kutokana na kutokuwa na uratibu.


Kauli mbiu ya mkutano wa wadau wa zao la muhogo Tanzania ni"Ongeza Tija,Tumia Fursa za Masoko,Muhogo Unalipa".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com