Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA MARA BAADA YA KUWASILI NAIROBI NCHINI KENYA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya leo tarehe 04 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wa nyimbo za Mataifa Mawili ya Tanzania na Kenya zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya leo tarehe 04 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya leo tarehe 04 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni Mara baada ya Kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya kuwasili Nairobi nchini Kenya leo 04 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wakielekea kwenye mazungumzo ya Pamoja na Ujumbe wa nchi mbili Tanzania na Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo ya pamoja na Ujumbe wa Kenya uliongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo tarehe 04 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo ya pamoja na Ujumbe wa Kenya uliongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo tarehe 04 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wakishuhudia Mawaziri wa Tanzania (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Michezo wa Kenya Balozi Amina Mohamed wakati wakisaini mkataba wa Mambo ya Sanaa katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama mara baada ya kuweka shada la maua kwenye Kaburi la Hayati Mzee Jomo Kenyatta Rais wa Kwanza wa Kenya lililopo jijini Nairobi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya. PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com