Sylivester Mwakitalu
**
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa taasisi za Serikali akiwemo Sylvester Mwakitalu kuwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kuchukua nafasi ya Biswalo Mganga ambaye ameteuliwa kuwa jaji wa Mahakama Kuu.
Taarifa ya uteuzi wa wakuu hao wa taasisi pamoja na wakuu wa mikoa ulioanza leo Jumamosi Mei 15, 2021 imetolewa leo na Mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu, Gerson Msigwa, ikieleza kuwa wataapishwa Mei 18, 2021 Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Inaeleza kuwa Rais Samia amemteua Neema Mwakalyelye kuwa Naibu mkurugenzi mkuu wa Takukuru na Joseph Pande kuwa naibu mkurugenzi wa mashtaka (DDDP).
Rais Samia pia amemteua Dk Edwin Mhede kuwa mkurugenzi mtendaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) kuchukua nafasi ya Ronald Lwakatale ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Nenelwa Mwihambi ameteuliwa kuwa katibu wa Bunge kuchukua nafasi ya Dk Stephen Kagaigai ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Soma pia
Social Plugin