MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amewatumia salamu mawakala wa wahamiaji haramu ambao wanatumia mkoa huo kuwapitisha na wale wanaopitisha dawa za kulevya kwamba wasijaribu kufanya hivyo maana watakachokutana nacho kitakuwa historia kwao.
RC Malima aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga ambapo alisema mkoa huo hautakuwa dezo ya kupitisha wahamiaji haramu na kama kuna watu wanadhani anatania wafanye hivyo waone watakumbana na jambo gani.
Alisema kwamba mkoa huo hautakuwa sehemu ya watu kupitisha mauzauza yao na wasijaribu kutokana na kwamba wamejipanga vilivyo kuhakikisha vitendo vya namna hiyo havifanyika kwenye mkoa huo huku akitoa onyo kwa wanaodhani wanaweza kujaribu.
“Ndani ya wiki mbili wahamiaji haramu wameongezeka naomba wasiufanye mkoa wa Tanga kuwa ni dezo ya wao kupitia na niwaambie kwamba Tanga hautakuwa mkoa wa kupitisha mauzauza yao na hata wale ambao wanafikiria kwamba wanaweza kupitisha dawa za kulevya wasijaribu zari kwani tumejipanga kuwashughulikia”Alisema
Alisema wahamiaji haramu hao wanapitia mkoa wa Tanga kwenda mikoa ya Pwani ,Dar,Bagamoyo kwa hiyo aliwataka waandishi wa habari kufikisha salama kwa wananchi kwa wale wanaojua wazi kwamba watu wanao wanashirikiana kwenye kusafirisha binadamu wanaowatoa mkinga wanawasafarisha usiku kwa usiku.
“Hao watu ambao wanao wanashiriikiana kusafrisha binadamu wanawatoa wilaya ya Mkinga kuwasafirisha usiku kwa usiku wengine wanapita Korogwe wanatoka Kilindi wanachana Korogwe hadi Handeni wanapitia Mkata wanaingia Pwani wengine wanatokea Mvomero pia eneo la Gairo hilo ni tatizo kubwa na hawawezi kufanikiwa kama hawana watu ambao wana shirikishiana nao”Alisema
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka waandishi wa habari mkoa wa Tanga wafikishe ujumbe kwamba wale wanaotumika kuwasafirisha huenda dhambi ya kusafirisha ni kubwa sana kuliko kusafirishwa.
Social Plugin