Wanamgambo wa Kipalestina wanasema wamerusha makombora 130 katika mji wa Israeli wa Tel Aviv baada ya shambulio la anga la Israeli kuangusha ghorofa katika eneo la ukanda wa Gaza.
Jumba hilo la ghorofa 13- lilishambuliwa saa moja unusu baada ya wakazi na wenyeji wa eneo hilo kushauriwa waondoke, shirika la habari la Reuters liliripoti.
Jeshi la Israel linasema kuwa linalenga wanamgambo mjini Gaza kujibu shambulio la awali la roketi.
Watu 31 wameuawa baadhi yao katika ghasia mbaya zaidi zilizowahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.
Jamii ya kimataifa imetoa wito kwa pande zote mbili kukomesha mapigano, yaliyofuatiwa na siku kadhaa za ghasia mjini Jerusalem.
Wanamgambo walikuwa tayari wafyatua mamia ya maroketi kuelekea upande wa Jerusalem na maeneo mengine.
Watu watatu wameuawa katika maeneo ya Israeli huku Wapalestina 28 wakiuawa kwa makomboro ya Israel.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu awali ailisema kundi kubwa la wanamgambo, Hamas, “limevuka mpaka” kwa kurusha maroketi kuelekea Jerusalem kwa mara ya kwanza ndani ya miaka kadhaa.
Hamas, ambayo inadhibiti Gaza, inasema imechukua hatua hiyo kulinda msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem dhidi ya “ dhalimu na ugaidi” wa Israel baada ya eneo hilo, takatifu kwa Waislamu na Wayahudi, kukumbwa na makabiliano kati ya polisi wa Israeil na Wapalestina siku ya Jumatatu na kusbabisha mamia kujeruhiwa.
Credit:BBC
Social Plugin