Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) imefanya maboresho ya ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) michezo ya viporo ambayo inazihusisha timu za Namungo FC na Simba ambao bado wana mechi nyingi mkononi.
Miongoni mwa maboresho hayo, TPLB imeupangia tarehe mpya mchezo wa watani wa Jadi, Simba na Yanga ulioshindwa kufanyika Mei 8, mwaka huu ambapo sasa utachezwa Julai 3, mwaka huu.
Taarifa iliyotumwa na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) leo Mei 16,2021 ambayo ni ratiba ya Ligi Kuu Bara imeonyesha tarehe mpya ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga ambao uliyeyuka mazima Mei 8, Uwanja wa Mkapa kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda.
Muda wa awali wa mchezo huo ulipangwa majira ya saa 11:00 ila muda mfupi kabla ya mchezo ratiba ilibdilishwa na kupelekwa mpaka saa 1:00 usiku jambo ambalo Yanga waligomea.
Yanga iliweka wazi kwamba ni lazima Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) kufuata kanuni kwa kuwa mpango huo ulikuwa ni kinyume na taratibu kuhusu kubadilisha muda.
Sasa watani hao wa jadi wanatarajiwa kukutana tena Uwanja wa Mkapa, Julai 3, Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.
Tazama ratiba hiyo hapa chini
Social Plugin