Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa[TAKUKURU]Wilaya ya Mpwapwa Bi. Julieth Mtui akimkabidhi fedha kiasi cha Tsh.Milioni mbili ,laki nne na sabini na tano elfu[ 2,475,000/= ] mzee mstaafu Benedict Mtihani alizodhurumiwa kutoka kwenye sehemu ya fedha zake za kiinua mgongo na kijana mmoja aliyekuwa akijihusisha na ukopeshaji wilayani humo.
***
Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania [TAKUKURU]Wilaya ya Mpwapwa imefanikiwa kurejesha kiasi cha Tsh.milioni mbili ,laki nne na sabini na tano elfu [. 2,475,000/= ] kwa mzee mstaafu Benedict Mtihani alizodhurumiwa kutoka kwenye fedha zake za kiinua mgongo na kijana mmoja aliyekuwa akijihusisha na ukopeshaji wilayani humo bila kufuata utaratibu.
Akizungumza na na Mtandao huu ,Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Mpwapwa Julieth Mtui amesema ofisi ya TAKUKURU Mpwapwa ilipokea taarifa kutoka kwa mzee mmoja mstaafu katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpwapwa masuala ya ulinzi alikopa kwa kijana anayejihusisha na mikopo umiza na baada ya fedha za kiinua mgogo kutoka kijana yule alimkata zaidi ya Tsh.milioni 11 kwenye akaunti ya benki kwani alikuwa ameshamnyang’anya kadi ya benki.
Mkuu huyo wa TAKUKURU ameendelea kufafanua kuwa,katika uchunguzi waliofanya walibaini kuwa fedha alizopaswa kulipa mzee ni pamoja na riba ni Tsh.Milioni nane laki mbili na elfu hamsini [8,250,000 ].
Hata hivyo mkuu huyo wa TAKUKURU ametoa ushauri kwa wastaafu na wanaotarajia kustaafu kujitahidi kwenda kwenye Taasisi zinazotambulika kisheria na kuwa na uelewa zaidi juu ya masuala ya riba na uhalali wa wakopeshaji hao.
Kwa upande wake Mzee Mstaafu Benedict Mtihani ameelezea jinsi alivyotapeliwa fedha za kiiunua mgongo huku akiipongeza TAKUKURU kwa kuweza kuokoa pesa zake.
“Kwa kweli nashukuru sana TAKUKURU kwa kuweza kunisaidia kuokoa fedha zangu ,niliambiwa na huyo kijana kuwa riba ya mkopo ni nzuri lakini nilinyang’anywa kadi ya benki baada ya mafao ya kiinua mgongo kutoka kakomba fedha zote kwenye akaunti”amesema
Social Plugin