Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TIC YATOA ELIMU KUHUSU UWEKEZAJI KUPITIA MAONESHO YA KIBIASHARA YA TANGA

 

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wao kwenye maonyesho ya Biashara Jijini Tanga leo
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji(TIC)  Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda kushoto akieleza masuala yanayohusu kituo cha Uwekezaji kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe (MB) alipotembelea Banda leo kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara ya 8
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda kushoto akieleza masuala yanayohusu kituo cha Uwekezaji kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe (MB) alipotembelea Banda leo kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara ya 8

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda katikati akiwa na watumishi wengine wa kituo hicho wakitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao

 KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda yaKaskazini kimeshiriki Maonesho ya Kibiashara ya 8 jijini Tanga kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu uwekezaji hapa nchini.

Maonesho haya kibiashara ya 8 yameandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuanzia tarehe 28 Mei na yanatarajiwa kuendelea hadi tarehe 6 Juni 2021 katika viwanja vya Mwahako jijiniTanga.

Maonesho haya yamekuwa yakifanyik ajijini Tanga kila mwaka yakiwa na lengo la kuhamasisha na kukuza biashara na uwekezaji mkoani humo na mikoa jirani na hivyo kuthibitika kuwa miongoni mwa maonesho yanayofanya vizuri katika kuhamasisha na kukuza biashara na uwekezaji, ubunifu, masoko, kuonesha fursa za uwekezaji na kusaidia ukuaji wa viwanda hapa nchini.

Akizungumza katika Banda la Maonesho la TIC, Meneja wa Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda alisema wamekuwa wakijitokeza kushiriki maonesho hayo katika kutekeleza Sheria ya Uwekezaji Na. 26 Sehemuya 6 (g) ambayo inakitaka Kituo cha Uwekezaji kufanya na kusaidia uwekezaji wa ndani kupitia shughuli mbalimbali za uhamasishaji ambazo ni muhimu katika kuhamasisha na kuwezesha kuongezeka kwa uwekezaji wa ndani.

Amesema Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Kaskazini kimetumia fursa hii kuelezea kwa umma majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Kituo hicho na fursa za uwekezaji zilizopo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini yaTanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Alizitaja miongoni mwa fursa zilizopo katika mikoa hii kuwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vya kuzalisha saruji, chokaa, madawa ya binadamu, madawa ya kilimo na mifugo, viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na yale ya mifugo kama nyama na maziwa.

Fursa nyingine za uwekezaji zilizopo katika mikoa hii ni pamoja huduma za utalii na ujenzi wa mahoteli ya utalii kutokana kuwepo kwa vivutio vingi vya utalii kama vile hifadhi ya mbuga zaSaadani, Mkomazi, Mlima Kilimanjaro, hifadhi ya mbuga ya Arusha, Serengeti, Manyarana Ngorongoro. 

Aidha, kuna fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo, ujenzi wa majengo yabiashara, usafirishaji, huduma za mashule na mahospitali, n.k.

Bw.Riganda amesema katika kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali zinazohusiana na uwekezaji kama vile cheti cha vivutio vya uwekezaji, huduma za upatikanaji wa ardhi, vibali vya ukaazi, vibali vya kazi, usajili wa makampuni ya biashara, ushauriwa kodi, masuala ya mazingira, ukaguzi na utoaji wa cheti cha ubora wa bidhaa, n.k, Kituo hicho kimewaleta maafisa mbalimbali kutoka katika taasisi na mamlaka za serikali ambao wanatoa huduma zote hizo pale pale TIC Makao Makuu kupitia huduma za mahala pamoja.

Upatikanaji wa huduma hizo umepunguza muda na gharama ambazo wawekezaji wangezipata kwa kuingia ofisi moja hadi nyingine.

Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Kaskazini kinatoa rai kwa wawekezaji wote wa ndani na nje kuzitumia fursa za uwekezaji ipasavyo kwa ajili ya maendeleo ya miradi yao na taifa kwa ujumla. Ofisi za Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Kaskazini zipo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Maonesho haya ya siku kumi yameweza kuvutia wafanyabiashara mbalimbali, wawekezaji, wajasiriamali (wachini na wakati) na asasi zisizo za kiserikali kutoka katika mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara. 

Miongoni mwa wawekezaji waliosajiliwa na TIC walioshiriki maonesho haya ya biashara jijini Tanga ni pamoja na Tanga Cement PLC (wazalishaji wa saruji ya Simba), D.D. Ruhinda and Company Ltd (wazalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyuzi za mkonge), Mamujee Products Limited (wazalishaji wa bidhaa za manukato), Harsho Group kutoka Kilimanjaro, Pee Pee Tanzania Limited (wazalishaji wa aina mbalimbali za mifuko ya kufungia bidhaa), makampuni ya uzalishaji wa chokaa, n.k.

Aidha taasisi mbalimbali za serikali pia zimetumia maonesho haya kuelezea huduma zao vikiwemo taasisi zinazotoa huduma wezeshi kwa wawekezaji kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Usajili wa Makampuni hapa nchini (BRELA), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Tanga, TCRA, n.k. Kauli mbinu ya maonesho haya mwaka huu inasema “Kilimo kwa Maendeleo ya Viwanda”.

Akizungumza namna walivyofaidika kupitia huduma za TIC, Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Harsho yaliyopo mkoani Kilimanjaro, Bw. Harold Shoo amesema wanajivunia sana kama wawekezaji wa ndani kuwekeza kwenye viwanda hususan katika kuzalisha vifungashio mbalimbali na vyakula vya mifugo. 

Wanasem abila TIC wasingeweza kukuza mitaji yao, kuingiza mitambo ya viwanda, na kuajiri wataalam wa kigeni ambao wamefanikisha sana uwekezaji hao.

 Hata hivyo wamelalamikia ucheleweshaji wa maombi ya vibali vya wataalam wakigeni ambao kwa namna moja au nyingine umekuwa ukiathiri maendeleo ya miradi yao.


Kituo cha Uwekezaji kimekuwa kikishiriki maonesho haya karibu kila mwaka ukitoa mwaka jana ambapo maonesho haya hayakufanyika kutokana na kuwepo kwa tishio la ugonjwawa COVID-19.

Maonesho haya  yamefunguliwa tarehe 31 Mei 2021 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Exaud Kigahe (MB).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com