Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TUME YA UTUMISHI WA UMMA KUTOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA KADCO

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TUME YA UTUMISHI WA UMMA KUTOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA KADCO

Tume ya Utumishi wa Umma inatarajia kutoa mafunzo  kwa Watumishi wa Kampuni ya Uendelezaji wa Kiwanja cha Ndege Kilimanjaro (KADCO) Mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji amesema kuwa mafunzo haya yameandaliwa na KADCO kwa lengo la kuwajengea uwezo Watumishi wa KADCO kuhusu Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Usimamizi wa Utendaji Kazi kupitia Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji kazi (OPRAS), kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia  Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia masuala ya Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma.

Mafunzo haya ya wiki mbili  yatafanyika kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 10 Mei, 2021 na yatafunguliwa Rasmi na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa George D. Yambesi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana na yatahitimishwa tarehe 24 Mei, 2021.

Bwana Muhoji amesema, Tume inatekeleza jukumu hili  kwa mujibu wa Kifungu cha 10 (1) ( C) cha  Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura 298.

          Imetolewa na:-       

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

TUME YA UTUMISHI WA UMMA

DAR ES SALAAM

07 Mei, 2021

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com