Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : BARRICK BULYANHULU YAWEZESHA WAJASIRIAMALI KUSHIRIKI MAONESHO YA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI KAHAMA


Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba (kushoto) na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu wakionesha bidhaa mbalimbali kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wajasiriamali zaidi ya 33 wanaotoka katika vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Dhahabu wa Barrick  Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wanashiriki katika Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji wilayani Kahama wakiwa na bidhaa zaidi ya 100.

Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yaliyoandaliwa na Taasisi ya GS1 Tanzania kupitia Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama yameanza leo Jumatatu Mei 24,2021 yatafikia tamati Mei 30,2021 katika viwanja vya Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama yakiongozwa na kauli mbiu ya ‘Nunua bidhaa za Kitanzania kuza uchumi wa nchi’.

Akizungumza wakati wa Maonesho hayo,Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba amesema mgodi huo umewaleta wajasiriamali wanaofanya shughuli zao katika Mgodi wa Bulyanhulu na nje ya mgodi kushiriki kwenye maonesho ili kukuza bidhaa, kupata masoko na kujifunza kutoka kwa wajasiriamali wengine ili kuongeza thamani ya bidhaa wanazozalisha.

“Miongoni mwa Wajasiriamali 33 waliowezeshwa na mgodi wa Bulyanhulu ni wale wanaojihusisha na kilimo cha mazao ya nafaka,mboga mboga na matunda, watengenezaji na washonaji wa nguo,wana mitindo, wafugaji wa kuku,wauzaji mayai,wafugaji nyuki,wataalamu wa kilimo na Kikundi cha Geka Hill chenye mradi wa kutokomeza mazalia ya mbu wanaosababisha Malaria.

Tumekuja na bidhaa zaidi ya 100 zinazozalishwa na wajasairimali hawa, tunapenda wapanue mawazo ya kibiashara na kuboresha bidhaa zao ili kujiinua kiuchumi”,ameeleza Dkt. Musiba.

“Wajasiriamali hawa ni sehemu ya shughuli za maendeleo ya jamii ya Mgodi wa Bulyanhulu ambao wamewezeshwa na mgodi kwa kupewa elimu kuhusu ujasiriamali na kwa wale wanaojihusisha na kilimo tuliwapatia mbegu,mbolea na dawa za kuulia wadudu ili walime mazao kibiashara zaidi”,amesema Dkt. Musiba.

Dkt. Musiba ameishukuru Taasisi ya GS1 Tanzania iliyopo chini ya Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama ambacho kipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuandaa maonesho hayo ili kuonesha bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa ndani ya nchi ambao pia watapata elimu ya kuongeza thamani ya bidhaa hizo.

Ameitaja changamoto inayowakabili wajasiriamali hao kuwa ni ukosefu wa mitaji hali inayowafanya washindwe kupata mikopo kwenye Benki hivyo wanaangalia namna ya kushirikiana na halmashauri ili wajasiriamali wapate mikopo yenye riba nafuu na isiyo na masharti magumu.

Nao baadhi ya wajasiriamali hao wamesema maonesho hayo yanawapa fursa ya kuonesha bidhaa wanazozalisha ambapo watapata elimu ya namna ya kufungasha bidhaa,urasimishaji biashara,kufungua fursa za masoko.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba akizungumza katika Banda la Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama leo Jumatatu Mei 24,2021 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba akizungumza katika Banda la Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama leo Jumatatu Mei 24,2021 
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba akionesha bidhaa zinazozalishwa na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba akionesha sabuni inayozalishwa na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba akionesha nguo iliyotengenezwa na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba akionesha matikiti yanayozalishwa na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba akionesha magimbi yanayozalishwa na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba (kushoto) akiangalia dawa za kutibu maradhi mbalimbali zinazozalishwa na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu  wakionesha nguo kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu  wakionesha nguo kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu  wakionesha nguo kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu, Dkt. Zumbi Musiba na Wajasiriamali akiangalia dawa ya kuua mbu inayotengezwa na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu  wakionesha nguo kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Mwananchi akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa mazao mbalimbali katika Banda la Wajasiriamali kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Mwananchi (kulia) akiangalia bidhaa zinazolishwa na Wajasiriamali kutoka vijiji 14 vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu  kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Mjasiriamali Kasanda James Chai kutoka Bufaso AMCOS Bugarama (kulia) akiwaelezea wananchi kuhusu kilimo bustani na mbogamboga kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Mjasiriamali Kasanda James Chai kutoka Bufaso AMCOS Bugarama (kushoto) akiwaelezea wananchi kuhusu kilimo mazao ya nafaka kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Wananchi wakiwa kwenye Banda la Wajasiriamali kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.
Mjasiriamali Mamuu Albert Makere kutoka Kampuni ya Mamuu Chicken akionesha mayai na kuku katika banda la Wajasiriamali kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com