Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Leopold Mosha
***
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waandishi wa habari wamekumbushwa umuhimu wa kuzingatia na kuchukua tahadhari za kiusalama wanapotekeleza majukumu yao katika kuihabarisha jamii.
Rai hiyo imetolewa leo Jumatano Mei 12,2021 mkoani Morogoro na Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Leopold Mosha wakati wa semina kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu iliyoandaliwa na THRDC.
Wakili Mosha amesema suala la usalama kwa waandishi wa habari ni la kuzingatia wanapotekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola,vyombo vyao vya habari na waandishi wa habari wenzao pindi wanapoona au kuhisi dalili za kuhatarisha usalama wao.
“Waandishi wa habari toeni taarifa pindi mnapoona usalama wenu upo hatarini. Usichukulie poa pindi unapoona usalama wako upo hatarini. Usikubali kitu kipite tu walau fanya jambo kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka mbalimbali ikiwemo vyombo vya dola, taasisi zinazohusu utetezi wa haki za waandishi wa habari na haki za binadamu kwa ujumla ikiwemo THRDC ili upate msaada”,amesema.
Social Plugin