Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMKE AOLEWA NA WANAUME SABA....KAWAJENGEA KILA MMOJA NYUMBA YAKE

Mwanamke huyo akiwa na wanaume zake
Mwanamke huyo akiwa na wanaume zake
**
Mwanamke mmoja ambaye ni Mganga wa Kienyeji nchini Nigeria ameweza kuolewa na wanaume saba tofauti, amesema wanaume wake hawawezi kumsaliti kwa sababu amewajengea nyumba ambazo ana uwezo wa kutembelea kimaajabu muda wowote wakitaka kumsaliti.

Mwanamke huyo amesema hayakuwa maagizo yake kuolewa na wanaume saba bali alipewa maagizo kutoka kwa wazee wake.

"Sikufanya kwa mapenzi yangu niliamriwa na wazee, ilikuwa ni agizo kutoka kwao na hapo ndipo nilipewa madaraka makubwa, Wazee waliniambia nizae watoto zaidi kutoka kwa waume zangu na nisiwe na mtoto mmoja kutoka kwa mwanamume mmoja, hiyi ndio sababu ya mimi kuoa zaidi ya waume sita"

Pia ameongeza kusema "Ilikuwa ya ajabu kwangu lakini ilibidi nitii vinginevyo ningeadhibiwa vibaya, wakati ninawaa-proach wanaume hawa walikuwa hawana chaguo zaidi ya kukubali kwa sababu ya nguvu zangu kuu"

"Nilijenga nyumba kwa kila mmoja wao na kuwatembelea wakati wowote, wakitaka kunisaliti ili kukidhi mahitaji yao, hawawezi kuthubutu kunidanganya nguvu zangu kuu zinanifikia kabla hawajafikiria".

Taarifa kama hii ya mwanamke kuolewa na mwanaume zaidi ya mmoja imetokea nchini Afrika Kusini kwa kusemekana wanawake wanaweza kuolewa na mwanaume zaidi ya mmoja.

Chanzo : Ghpage.com, Instablog9ja, Browngh.com, Minutegoal.com, Larc.org.na, Gistsbaste.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com