Waziri Mkuu Majaliwa awasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha


 Waziri Mkuu, Mheshimwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu,  Mkaguzi  Msaidizi pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha  za umma zinazowakabili.

Akizungumza katika Kikao Kazi na Waziri wa Fedha na Mipango, Kaibu Mkuu,Manaibu  Katibu Wakuu na Watendaji Waandamizi wa Wizara hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Mei 27, 2021,  Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi ACP Salum Rashid Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika kwamba tuhuma si za kweli wahusika watarejeshwa kazini.

Mheshimiwa Majaliwa alizitaja baadhi ya tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika  Machi 31, Mwaka huu  kupitia vocha 30 ya sh.milioni 251  yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi hiyo maalum ni kazi gani na nani aliifanya hiyo kazi.

Amesema  siku hiyo hiyo  ya Machi 31 pia zililipwa  sh. milioni 198.8 kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mheshimiwa Majaliwa  amesema Aprili 8 mwaka huu watumushi  27 wa  Wizara hiyo walilipwa sh. milioni 44.5 zikiwa ni posh ya kazi maakum ya wiki nne. Pia  Aprili 13 mwaka huu zililupwa sh. Milioni 155.2 kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya ya kazi maalum ya wiki tatu.

Aidha, Aprili 30 mwaka huu zililipwa sh. milioni 43.9 kwa ajili ya kuandaa  mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyo hiyo zililipwa sh  miloni 14.4 kwa ajili ya siku ya wanawake. Fedha nyingine sh. Milioni 43 zililipwa siku hiyo na kufanya  jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa shilingi mikioni101.8.

Amesema kuwa, mei 1 asubuhi mwaka huuzililipwa  sh. milioni 184.1 na mchana zililipwa sh  milioni 264 zikiwa ni malipo ya kazi maalum. "Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho"

Aliongeza kuwa Mei 3 mwaka huu zililipwa sh. milioni146.5 kwa  watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa Mpango Kazi wa Manunuzi kazi ambayo  ni sehemu ya majukumu yao ya jila siku.  Tarehe hiyohiyo zililipwa  sh. milioni 171.2 kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Mheshiniwa Majaliwa  amesema sh. milioni155 zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi. " Yaani hii kazi ya ukaguzi ineliowa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani,  na sijaongekea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha  kisha mnakwenda kuzichukuwa huko mlikozihamishia."

Mheshimiwa Majaliwa amewataka watendaji wa Wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na alitahadharisha kuwa watakaoendekea kuchen na pesa za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha, Waziri Mkuu aliwapongeza watendaji wengine wa wizara hiyo ambao wameendelea kufanya kazi kwa weledi “na nimesema hapa si wote wenzenu wachache wanatumia vibaya nafasi zao kutuchafua wizara ya fedha”

MWISHO.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post