Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, akizungumza kwenye mkutano wa dini na wanajumuiya hiyo katika Msikiti wa Wigehe Manispaa ya Kahama.
Na Marco Maduhu, Kahama
Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya, imeendesha mkutano mkubwa wa kidini wa mwaka katika viwanja vya msikiti wa Ahmadiyya uliopo Wigehe Manispaa ya Kahama.
Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na viongozi wa Jamaati, na Masheikh wa jumuiya hiyo ya Ahmadiyya kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, na kuongozwa na Amir na Mbashiri Mkuu wa Ahmadiyya Tanzania Shekh Tahir Mahmood Chaudhry.
Sheikh Chaudhry akizungumzia lengo la mkutano huo, amesema dhumuni lake kubwa ni kutoa mafundisho ya kidini kwa wana jumuiya, pamoja na kuwafanya wawe raia wema wenye kuishi kwa upendo na kudumisha amani ya nchi.
Amesema Jumuiya hiyo ya Waislam Ahmadiyya, imekuwa ikiendesha mikutano mikubwa kila mwaka hapa nchini, ili kuwafanya wanajumuiya hiyo kuishi kwenye miongozo ya kidini.
"Jumuiya yetu ya Waislam Ahmadiyya tunaata wana jumuiya wawe watu wema, na siyo kuwa watenda maovu wala kujihusisha kwenye masuala ya ugaidi na migomo, sababu dini yetu hairuhusu kufanya fujo bali ni kuishi kwa amani,"amesema Sheikh Chaudhry.
Pia amesema Jumuiya hiyo inapinga sana vitendo vya baadhi ya wananchi kuendekeza masuala ya imani potofu za kishirikina, hasa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, na kusababisha mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, wazee na wenye Ualbino.
Katika hatua nyingine Chaudhry amesema, mbali na jumuiya hiyo kutoa mafundisho ya kidini na hata kujenga Misikiti 21 mkoani Shinyanga, pia wamekuwa wakichangia huduma za kijamii ambapo wamejenga visima vya maji 150 mkoani humo, ili kuwaondolea wananchi changamoto ya ukosefu wa maji salama.
Kwa upande wake Sheikh wa Jumuiya ya waislam Ahmadiyya kutoka mkoani Mbeya Karim Shams, aliwataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema, pamoja na kufuata misingi ya kidini.
Nao baadhi ya wanajumuiya hiyo ya Ahmadiyya waliohudhuria mkutano huo wa kidini, walisema mafundisho hayo yamekuwa msaada mkubwa sana katika imani zao.
Tazama picha hapa chini.
Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, akizungumza kwenye mkutano wa dini na wanajumuiya hiyo katika Msikiti wa Wigehe Manispaa ya Kahama. Picha zote na Marco Maduhu
Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry,akiendelea kuzungumza kwenye mkutano huo.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya kutoka Jijini Mbeya, akizungumza kwenye mkutano huo wa kidini.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya kutoka Iringa Riag Ahmed Dogani, akizungumza kwenye mkutano huo wa kidini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya mkoani Shinyanga Yusuf Mgeleka, akizungumza kwenye mkutano huo wa kidini.
Hassani Harona akimwakilisha katibu wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Kahama, akizungumza kwenye mkutano huo wa kidini.
Waumini wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya wakiwa kwenye mkutano huo wa kidini.
Waumini wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya wakiwa kwenye mkutano huo wa kidini.
Waumini wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya wakiwa kwenye mkutano huo wa kidini.
Viongozi wakiwa mweza kuu.
Viongozi wakiwa meza kuu.
Waumini wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya wakiwa kwenye mkutano huo wa kidini.
Waumini wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya wakiwa kwenye mkutano huo wa kidini.
Awali Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, akipandisha Bendera ya Jumuiya hiyo kwenye eneo la mkutano, pamoja na bendera ya Tanzania kwa nusu mlingoti kwa ajili ya kuomboleza msiba wa Hayati aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda.
Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, akiongoza Swala kwenye mkutano huo wa kidini.
Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, akiongoza Swala kwenye mkutano huo wa kidini.
Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, akiangalia vitabu vyenye mafundisho ya dini ya kiislam kwenye eneo hilo la mkutano.
Awali Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, akiwasili kwenye eneo hilo la mkutano wa dini, katika viwanja ya Msikiti wa Wigehe Manispaa ya Kahama.
Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya dini ya Waislam Ahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, wasita kutoka kushoto, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa jumuiya hiyo kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Na Marco Maduhu- Kahama.
Social Plugin