Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BASI LA CLASSIC LAPATA AJALI KONA YA DIDIA SHINYANGA..LAUA NA KUJERUHI


Na Mwandishi wa Malunde 1 blog, Shinyanga

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Kampuni ya Classic lenye namba za usajili binafsi Salum Rashidi Classic (SRC 3), likitokea Kampala nchini Uganda kwenda Jijini Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 10 alfajiri katika Kona ya Didia wilayani Shinyanga,na kusababisha vifo vya abiria hao na majeruhi 20.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba, amewataja watu waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Wahida Yusuph mkazi wa Pemba, Joseph Joseph mkazi wa Dar es salaam, Rehema Haji mkazi wa Unguja, na Nasorro Hamisi mkazi wa Zanzibar.

Amewataja majeruhi watano ambao wamekatika viungo vya miili yao, kuwa ni Njama Hassani, Fatuma Kesi, Sada Manga, na Twalibu, wote wamekatika mkono wa kushoto na mmoja mguu wa kulia, pamoja na Mohamed Daudi mkono wa kulia.

Aidha amesema majeruhi wengine 15 walitibiwa na kuruhusiwa, na hali zao zinaendelea vizuri, na kubainisha kuwa basi hilo lilikiwa na abiria 43 ambapo wengine ni wazima hawakuumia.

"Chanzo cha ajali hii ni mwendo kasi, ambapo Dereva wa basi anayejulikana kwa jina la Maxison Mkuru alishindwa kukata Kona na kusababisha ajali, na tunamsaka kwa sababu amekimbia," alisema Magiligimba.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya majeruhi wamesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya dereva kushindwa kuimudu kona ya Didia.

Soma zaidi Hapa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com