Mwanaume mmoja wa nchini Uhispania amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kumuua mamake na kula mabaki yake.
Alberto Sanchez Gomez mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa 2019 baada ya maafisa wa polisi kupata mabaki ya mwili katika nyumba ya mamaake huku mengine yakiwa katika plastiki.
Mahakama ilikataa kwamba alikuwa anakabiliwa tatazo la kiakili wakati wa mauaji hayo.
Atatumikia kifungo cha miaka 15 kwa mauaji na miezi mingine mitano kwa uharibifu wa mabaki ya mfu. Pia ametakiwa kulipa faini $73,000 kama fidia.
Maafisa wa polisi waliwasili katika nyumba hiyo Februari 2019 baada ya rafiki kuwasilisha malalamishi kwa wakfu wa Maria Soledad Gomez ambaye alikuwa na umri wa miaka 60.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, mahakama ilielezewa kwamba Sanchez , wakati huo akiwa na umri wa miaka 26 alimnyonga mamaake wakati wa mzozo.
Baadaye aliukatakata mwili wa mamake na kuula huku vipande vingine akiwalisha mbwa.
Vyombo vya habari vya Uhispania vinasema kwamba alikuwa anajulikana na maafisa wa polisi kutokana na ghasia dhidi ya mamake na kwamba alikuwa amekiuka agizo la kumkamata wakati alipokamatwa.
Chanzo - BBC SWAHILI
Social Plugin