Mwanachama wa Chadema na mwanazuoni, Profesa Mwesiga Baregu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Juni 13, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es salaam wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Profesa Baregu alikuwa mhadhiri wa sayansi ya siasa na utawala wa umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baadaye alisitishiwa mkataba wake kwa kile kilichoelezwa kuchanganya utumishi na siasa. Baadaye alihamia Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) jijini Mwanza.
Alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema hadi mwaka 2019.
Social Plugin