Kampuni ya Barrick, kupitia mgodi wake wa North Mara, imetunukiwa tuzo kwa kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji (Investment Guide ) mkoani Mara uliofanyika katika viwanja vya Mwembeni Complex, mjini Musoma ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhshimiwa Kassim Majaliwa.
Mhe. Kassim Majaliwa, alitumia nafasi hiyo ya kuzindua mwongozo kwa kuwakaribisha wawekezaji kuchangamia fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani humo na kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya 6 itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchi ma kuondoa vikwazo vinavyozorotesha uwekezaji.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel ,alishukuru wadau mbalimbali waliofanikisha maandalizi ya uzinduzi huo ikiwemo kampuni ya Barrick kupitia mgodi wake wa North Mara.
Kwa kutambua mchango huo kampuni Waziri Mkuu,Mh.Kassim Majaliwa ilkabidhiwa tuzo na cheti kwa watendaji wa mgodi wa Barrick North Mara.
Mbali na kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji, Barrick imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kuboresha uchumi wa kijamii ikiwemo kukabiliana na changamoto mbalimmbali za kijamii hususani katika sehemu zinazozunguka maeneo yake ya kazi.
Mchakato wa Serikali kuanzisha mpango wa kila mkoa kuzindua Mwongozi wa uwekezaji umelenga kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo,ili kuvutia wewekezaji wa nje,kukuza biashara katika mikoa hiyo hayo na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii.
Uzinduzi huo umekuwa ukifanyika sambamba na maonyesho ya bidhaa ya wajasiriamali na makampuni kwa ajili ya kutagaza biashara na shughuli zao mbalimbali.
Social Plugin