Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akijibu swali Bungeni leo Jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine amesema Bonde la Pori tengefu la Mto Kilombero ni muhimu Kitaifa na Kimataifa kutokana na uhifadhi wa bionuwai zilizo adimu Duniani kama vile mnyama aina ya sheshe.
*******************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja amesema Bonde la Pori Tengefu la Kilombero ni sehemu ya ardhioevu linalochangia asilimia 62.5 ya maji yote ya mto Rufiji hivyo kuwa chanzo muhimu cha maji kwa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere.
Amesema Bonde hilo lina umuhimu kitaifa na Kimataifa kutokana na uhifadhi wa bionuwai zilizo adimu Duniani kama vile mnyama aina ya sheshe.