Albert Chalamila
*
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Juni 11,2021 amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa na kuteua wengine. Katika mabadiliko hayo , Mkuu wa Mkoa wa Mara , Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi anahamia Mkoa wa Mwanza ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila uteuzi wake umetenguliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Hapi anahamia mkoa wa Mara na aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Balozi Dkt. Batilda Salha Buriani anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora huku aliyekuwa Katibu Tawala wilaya ya Simanjiro, Zuwena Omari Jiri anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
Social Plugin