CHALAMILA AKABIDHI OFISI KWA RAS MPYA MWANZA MHANDISI ROBERT GABRIEL
Friday, June 11, 2021
Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila alikabidhi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi leo masaa machache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Juni 11,2021 kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa na kuteua wengine.
Katika mabadiliko hayo , Mkuu wa Mkoa wa Mara , Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi anahamia Mkoa wa Mwanza ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila uteuzi wake umetenguliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Hapi anahamia mkoa wa Mara na aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Balozi Dkt. Batilda Salha Buriani anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora huku aliyekuwa Katibu Tawala wilaya ya Simanjiro, Zuwena Omari Jiri anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin