Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Ramadhani Kingai amesema chanzo cha ajali hiyo ni ulevi na kwamba wanamshikilia dereva wa gari hilo.
“Inaonekana dereva alikuwa amelewa wakati akiendesha gari liliacha njia na kuingia mtaroni eneo la Tanganyika Packers karibu na sehemu ambayo Mchungaji Boniphace Mwamposa huwa anatoa neno, mtangazaji, Fredwaa alifariki ila dereva tunamshikilia” amesema Kingai.
Amesema kwa mujibu wa taarifa hata Fredwaa hakuumia ila inaonekana alipata mshituko kwani dereva hajaumia.
Fredwaa alijizolea umaarufu katika kipindi chake cha asubuhi pale Radio Free Africa jijini Mwanza, ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa na segment inaitwa Vodacom Top Five.
Fredwaa baada ya kuhamia Clouds Fm akitokea RFA alikuwa akisikika sana katika kipindi cha asubuhi Power Breakfast, akiungana na Mbwiga, Gerald Hando, Bonge na wengine.
Wakati wa uhai wake, Fredwaa pia amewahi kufanya kazi Times Fm.
R.I.P Fredwaa
Social Plugin