RAIS wa kwanza wa Zambia, Dk. Kenneth Kaunda amelazwa katika Hospitali ya Maina Soko jijini Lusaka kufuatia maradhi yanayomsumbua kwa siku kadhaa sasa.
Taarifa iliyotolewa na ikulu ya nchi hiyo, imeeleza kwamba jopo la madaktari wanafanya kila kinachowezekana kumtibu muasisi wa taifa hilo na kuwaomba Wazambia na jumuiya za kimataifa kuendelea kumuombea ili apone.
Kaunda aliyezaliwa April 28, 1924, aliitawala Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1991.
Social Plugin